Showing posts with label KUMBU KUMBU. Show all posts
Showing posts with label KUMBU KUMBU. Show all posts

3 July 2012

Kama si bandama basi nini?


Ukiwa unafanyiwa  operesheni ukazinduka ghafla ukasikia Dokta akisema chochote kati yafuatayo, ujue operesheni yako imeshakuwa soo….

-       Aise ukurasa 43 wa maelezo haupo sasa tuimprovise?

-       Hicho kinyama msikitupe kitatusaidia kutoa maelezo kwa nduguze

-       Nesi hii haiwezi kuwa bandama, maana kama hii bandama hii huku chini itakuwa nini?

-       Nani kanionea saa yangu?

-       Nimepoteza mkasi




Heri ningebaki hospitali

Dokta alienda kuwinda, aliporudi wenzie wakamuuliza
MADOC: Vipi aise umeua nini huko?
DOC MUWINDAJI: Hakufai kabisa, sikuua kitu chochote heri ningebaki hapa hospitali

Nilikwambia usimwambie



Mdada 1: Sasa imekuwaje tena? Mbona umemwambia kuwa nilikwambia na nilikwambia usimwambie nilikwambia?
Mdada 2: Hee amekwambia? Mi nilimwambia asikwambie kuwa we ulinambia
Mdada 1: Haya basi tena, sasa usimwambie kuwa nimekwambia amenambia

Kiti anamtaka mganga

Jamaa mmoja bonge ya mtu alikuwa na matatizo ya akili, ndugu zake wakampeleka kwa mganga. Mganga akafanya vibwanga vyake mgonjwa akapandisha shetani, akawa mkorofi hashikiki, huku akipiga kelele,
MGONJWA:Nataka nataka nataka
MGANGA: Unataka nini?
MGONJWA: Nataka nataka.
MGANGA: Sema unataka nini tukupe utulie?
MGONJWA: Mganga nataka kulala na mganga
MGANGA: Umesema?
MGONJWA: Nataka kukuoa wewe.......mganga akatimua mbio vibaya sana