Mdada mmoja mke wa mtu
alikuwa akisumbuliwa sana na jamaa mmoja aliyekuwa akimtaka kila siku, hatimae
akamwambia mumewe. Mume akamwambia mkewe, we mkubali tu, ila mwambie aje mlale
hapa kwetu, mi ntajificha uvunguni na panga. Akisha ingia ukiona kamaliza kuvua
nguo we ning’iniza mkono anza kuuchezesha, mi nikiuona ntatoka uvunguni na
kumfunza adabu.
Mdada akafuata masharti
ya mumewe na hatimae wakaingia chumbani na yule bwana , mumewe akiwa tayari na
panga uvunguni mwa kitanda. Jamaa alipovua shati, mke alishangaa kuona ana
makovu makubwa kifuani na mgongoni;
MKE: He mbona una
makovu hivyo
JAMAA: Niwe mkweli mie
nina tatizo sana la kupenda wake za watu, waume wengi wamekuwa wakipanga
kunifumania, nimeshafumaniwa mara kumi na tisa, na wote walionifumania nimewaua.
MKE: He jamani….jamaa
akaendelea kuvua nguo alipomaliza mdada akaanza kuning’iniza mkono ili mumewe
atoke uvunguni, mume kabana kimya, kila jitihada za mdada kupunga mkono
hazikupata majibu mpaka jamaa kamaliza shughuli zake akatokomea.
MKE: Jamani sasa ndio
nini? Mbona hukutoka
MUME: We we we, mwenyewe
umesikia kasha ua 19 unataka niwe wa ishirini?
Hahahahaaaa hiyo kiboko!
ReplyDelete