4 July 2012

Baba, mlete mbwa afundishwe kusoma

Jamaa kaingia chuo katikati ya simesta kaishiwa akamuandikia baba yake barua. 'Chuoni mambo mazuri sana, kuna maajabu hapa maprofesa hapa wamegundua njia ya kufundisha mbwa kuongea, mlete Bobi na shilingi laki 5, baada ya muda atakuwa anaweza kuongea. Mzee wa watu haraka akatuma mkwanja na mbwa, haikuchukua muda mkwanja ukaisha. Denti akamtumia baba yake barua nyingine kuwa wameboresha program sasa wanaweza kumfundisha mbwa kusoma, mzee aongeze kimilioni tu. Mzee wa watu aliyekuwa tayari anajisifu kijiji kizima akauza ng'ombe akatuma mkwanja. Likizo ikafika Denti akabaki anawaza anaenda kumwambia nini baba yake. Alipofika tu baba yake akamuulizia Bobi wake. Denti akamuita baba yake pembeni,' Baba hili nitakalokwambia sitaki mama asikie'. Baba akauliza,'Vipi tena?'. Denti akaanza,' Jumapili iliyopita tumeamka vizuri na Bobi, yeye kama kawaida yake akaenda kuchukua gazeti la Mzalendo na kukaa kwenye kiti na kuanza kusoma, ghafla wakati anasoma akaniita akanambia hivi baba yako bado anaendelea na kale kachangudoa ka pale mtaa wa pili? Nilishtuka'. Baba akaingilia kati,'Ungemuua hapo hapo mbwa mshenzi huyu anataka kuniharibia mambo yangu?', Denti akajibu,'Baba na mimi lilinijia wazo hilohilo sikumchelewesha nikamtwanga nyundo ya kichwa'. Baba akamsifu mwanae'Safi sana safi sana mwanangu'

No comments:

Post a Comment

SEMA USIKIKE