Jamaa alimkuta mwanamke mmoja pale
Ferry analia, akamuuliza shida, yule mdada akasema maisha yamemshinda anaona
heri ajiue. Jamaa akamwambia kuwa yeye ni baharia kwa hiyo akikubali atamuweka
kwenye boksi kisha atamficha kwenye meli yake na wataweza kusafiri mpaka Ulaya
wakifika huko atamuoa. Bibie akaona heri hilo akaingia kwenye boksi jamaa
akambeba na kweli mdada akajikuta yuko kwenye stoo moja wapo katika meli, jamaa
akawa anamletea chakula kila siku na mara nyingine yeye mwenyewe analala huko
kwenye hako kastoo,akimhakikishia mdada kuwa wanakaribia visiwa vya Komoro, na
kisha hutoka na kuendelea na shughuli. Ilipita wiki ndipo yule mdada
akagundulika na nahodha wa chombo hicho, alipoulizwa akalazimika kueleza kila kitu,
na kuwa anamuomba nahodha asimtupe baharini bali amlinde mpaka watakapofika
Ulaya. Nahodha akamwambia mdada, 'Wala usipate taabu sikutupi popote, ila jamaa yako
kakudanganya hii si meli ya kwenda Ulaya ni pantoni ya kwenda Kigamboni,
tukifika huko shuka'
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE