Jamaa yangu Devi
hana raha, mchana leo alipigiwa simu na Bosi wake ambae alikuwa safari, yeye mwenyewe wakati huo alikuwa bar akipata moja moto moja baridi saa za kazi;
Bosi: Vipi Devi?
Mnaendeleaje na kazi hapo ofisini?
Devi: Mkuu hapa
mambo safi sana tuko bizi sana, watu leo wamekuwa wengi utafikiri wametumwa bosi, hakuna hata nafasi ya kupumua
Bosi: Ok, Unaweza
kunisaidia kitu kimoja?
Devi: Hakuna
tabu Mzee sema tu.
Bosi: Haya maliza hiyo bia yako, halafu nenda kaunta niulizie bili yangu changanya na bili yako
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE