Toka kwa Anko Tom wa Tanzania Daima…………JUMATATU ya
wiki iliyopita nilikwenda katika ofisi moja jijini Dar es Salaam ambayo mara
kwa mara huwa nafika hapo kutokana na shughuli zangu za kila siku za kutafuta
riziki.
Mara baada ya kufungua mlango wa ofisi hiyo
nilikaribishwa na bonge la zogo hivyo nikajikuta nimeduwaa kwa muda wa dakika
kadhaa nikiwa sina la kufanya zaidi ya kuwaangalia na kuwashangaa hao waliokuwa
wakizozana.
Zogo hilo liliendelea hadi pale mwanadada mmoja
aliyekuwa na muonekano wenye sifa zote za mtu mtanashati na mstaarabu
alipoondoka ndipo hali ya hewa ya ofisi hiyo ilipotulia na mimi nikapata nafasi
ya kuuliza ili nipate kujua sababu za kutokea kwa zogo hilo ambalo nina hakika
kama isingekuwa ni sehemu ya ofisi za serikali, basi lazima sisi wapenda mchezo
wa masumbwi tungepata burudani hiyo bila ya kulipa kiingilio chochote.
Nilipoelezwa sababu za ugomvi huo kuwa ni wizi wa
tishu (karatasi za chooni) kwa hakika nilishindwa kuamini kama kweli huyo
bibiye aliyetoka hapo ndiye mtuhumiwa mwenyewe au kasingiziwa!
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE