Sharobalo katoka kwenye mnuso amelewa njwii,
kaondoka huko na chupa nyingine za Nyagi kaweka mifuko ya nyuma ya KATA K yake.
Sababu ya ulevi alipofika karibu na kwake akateleza akaangukia makalio chupa
zikavunjika na kumchanachana makalio. Akajikongoja mpaka ndani kwakwe, alipovua
suruali akaamua kujitibu kwa kubadika plasta kwenye vidonda, basi kwa msaada wa
kioo cha kabati lake akawa anajiaangalia palipo na kidonda na anabandika
plasta. Hatimae akaona amefanya kazi nzuri akajitosa akalala...... Asubuhi
alipoamka, akashangaa kioo chote kimebadikwa plasta na makalio yanauma
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE