Katika maisha yangu nimekwisha sikia vituko vingi kuhusu bangi. Nikikumbuka siku ya kwanza nimemuona rafiki yangu akivuta bangi(1968), jina lake ni Iddi sitataja majina mengine ameshakuwa mtu mzima sasa ninauhakika anawajukuu wengi tu. Alikuja mahala ambapo tulikuwa tunafanya mazoezi ya muziki maana naye alikuwa mpiga gitaa mzuri, akatoa bangi kwenye kibox cha njiti za kibiriti akasokota akavuta, wote tukimkodolea macho na kusubiri apagawe, hakuna cha ajabu alichofanya ila tu nakumbuka alikuwa anarudia rudia na kudai sisi sote ni samaki. Mpaka leo nikikutana nae huwa namtania, 'samaki'. Rafiki yangu mwingine ambaye ana wadhifa mkubwa serikalini aliwahi kunambia kuwa kuna siku alivuta bangi akahisi shati lake lina siafu, ilibidi alitoe na kulitupa pembeni huku akipiga kelele 'siafu siafu'. Kuna Mzee mwingine Richard, ambaye kwa sasa mawasiliano yetu yamekuwa ni kupitia FB maana miaka mingi hatujaonana, aliwahi kuwa kituko shuleni baada ya kuvuta bangi wakati wa mapumziko ya saa 4, enzi hizo akiwa form 2, yeye alihisi mbingu zinateremka na kuja kumbana, kwa hiyo nae akazidi kutembea huku akiwa ameinama macho yake juu, akiangalia mbingu ambazo kwake zilikuwa zinateremka na kukaribia kumbana, watu wote tukimuangalia na kumshangaa. Sitasahau nilivyocheka kituko cha rafiki yangu marehemu aliyekuwa mwanamuziki muimbaji, ambaye alinambia yeye na rafiki zake mara nyingi walikuwa wanazungumza kuwa kuna wauza bangi huchanganya bangi na kinyesi cha binadamu ili iwe kali zaidi. Sasa siku moja wenzie walipompa kipisi cha bangi, kilianza kumletea hisa za kufa kufa hivyo akahisi 'wamemchanganyia'. Kadri muda ukivyozidi ndivyo alivyozidi kujisikia vibaya, ikalazimu akimbilie kwa baba yake huku akilia,'Baba baba wamenichanganyia'
..sasa Kitime kuna kali ya ukweli ya muuza vinyago(kaajiriwa)..yeye alikuwa anauza vinyago vya kawaida vya mpingo..sasa siku moja akavuta bangi kwa mara ya kwanza tena asubuhi kabla ya kwenda kazini...ila sasa bosi wake jana yake usiku alileta vinyago kutoka Congo(vya kizamani)ambavyo mara nyingi hutoa harufu mbaya sana(sijui kwanini)..sasa jamaa asubuhi akiwa "high"(kwamara ya kwanza) kafungua duka, kasikia harufu mbaya sana, basi akampigia bosi wake;
ReplyDeleteJamaa;bosi huku hali ni mbaya sana
Bosi; kwani kuna tatizo gani?
Jamaa:hawa wanyama wote wamekunya humu dukani yani kunanuka kimba balaa njoo mwenyewe uzoe mavi mimi kazi yako basi...
Daah nimecheka sana😂
ReplyDelete