12 July 2012

Wakata nyonga tuko wengi

Pamoja na maneno mengi yatakayoanza lakini ukweli ni kuwa wengi wetu tungeweza kupata kazi ya kucheza show Twanga, Extra bongo au FM Academia bila wasiwasi. Najua wabishi wataanza kusema ohhh mie siwezi, si kweli mbona kila siku unafanya mazoezi ya kukata nyonga tena bila kulazimishwa. Haya kama mi muongo, Je unaweza kupiga mswaki bila kukata nyonga? Kajicheki peke yako bafuni halafu njoo utuambie ukweli wako hapa ukutani

No comments:

Post a Comment

SEMA USIKIKE