Haya Jeshi la Kuienga Taifa (JKT), ndio
hilo linakuja tena. Kwa kweli ni mahala ambapo wengine watapafurahia wengine
watakesha wanalia, lakini mwisho kila mmoja atatoka na kitu kipya na kumbukumbu ya pekee katika maisha. Lakini JKT
ina masharti mengi, kwa hiyo nimeona nianze kutoa WARAKA WA KWANZA KWA MAKULUTA’ ambao utaweza kuwasaidia ‘
makuluta’ watarajiwa kupata ahueni wakienda huko. Jambo la kwanza kuanzia siku
utaingia katika eneo la kambi wewe utaitwa KURUTA, hili ni neno lililotokana na
neno la Kiingereza ‘recruit’, usipaniki ukadhani linatoka kuleee pande
anazotoka Lady nanihii wa Machozi. Ukifika utapewa namba na utajulikana kwa namba yako.
Kila utakapofungua mdomo wako lazima umalize na neno AFANDE. Ukiulizwa unatoka
wapi? Utajibu Dar es Salaam AFANDE, ukiulizwa uko Coy gani? utajibu,Coy A
AFANDE, kimsingi utalitaja hilo neno mara nyingi mpaka hata usingizini utakuwa
unaliota, usishangae ukitoka huko, hata demu wako akikuuliza ,’Bado
unanipenda?” utajikuta unajibu, Ndio AFANDE. Lakini ni muhimu kuwa na akili na kujichunga sana
ukiulizwa jina lako hasa kama jina lako ni Rungula, Mboya, Kichacha na majina
kama hayo ambao ukiunganisha lile neno la AFANDE maana inaweza kuwa nyingine
kabisa na ukaishia kupata adhabu kwa kusema kitu cha ukweli, kwa mfano ukiwa
unaitwa Kichacha, ukaulizwa, Jina lako nani? Ukijibu Kichacha afande, unaweza
ukaishia mahabusu, hivyo basi ni vema kukarabati majina ili yasilete
utata. Katika waraka wangu wa pili italazimika niwaeleze msamiati wa JKT ili muweze kufahamu maana ya maneno kama , Jongomeo, Maslahi, Disko na kadhalika
Wasalaam ni mimi Afande
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE