Jamaa watatu walienda
kuomba tenda ya kujenga uzio wa nyumba ya serikali,
MJENZI 1: Mimi naweza kujenga uzio kwa shilingi
milioni 2, vifaa milioni,wajenzi laki tano na mimi nitapata faida laki tano.
MJENZI 2: Mimi nanaweza kujenga uzio huo kwa shilingi
milioni tatu, vifaa milioni, wajenzi milioni na mimi mwenyewe ntapata faida ya milioni.
Mjenzi wa tatu akamwita pembeni mtoa tenda,
MJENZI 3: Sikiliza mkuu mi nataka milioni 12, milioni
tano zako, tano zangu halafu tunamkodisha yule fala wa kwanza ajenge uzio,
imekaaje hiyo? Akapata tenda mara
moja.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE