27 September 2012

HAWEZI KUNIOA SI 'TYPE' YANGU

Dear Mzee Cheka Na Kitime,
Nategemea barua hii itakukuta salama. Mimi ni msichana wa miaka 23. Nilifiwa na wazazi wangu wakati nikiwa na miaka minane. Bibi yangu alishindwa kunilipia shule hivyo nikawa nyumbani tu, bahati nzuri mvulana mmoja kijijini kwetu akanambia atanisaidia, wakati huo alikuwa anauza machungwa barabarani. Kweli alianza kunilipia shule, miaka yote, hatimae hata yeye akabadili kazi akaanza kuendesha daladala, na ameendelea kunilipia mpaka sasa niko chuo kikuu. Namshukuru Mungu kwa kunikutanisha na malaika kama huyu sijui siku hizi ningekuwa wapi
Tatizo langu ni kuwa anataka kunioa nikimaliza chuo, na mimi kwa kweli nashindwa kumwambia kuwa itakuwa vigumu kwa kuwa yeye siyo 'type' yangu. Hebu fikiria mimi ni graduate halafu naolewa na dreva wa daladala, ni wazi kuwa si type yangu. Ninachoomba ni busara zako ntamwambiaje bila kumuumiza, kuwa haiwezekanai mimi nikaolewa na yeye?

No comments:

Post a Comment

SEMA USIKIKE