Katika
jamii ya binadamu wa Bongo kuna hawa wanaoitwa ‘DOMO ZEGE’. Kutokana na ubaguzi wa hali ya juu wa
kijinsia jina hili linahusu
wanaume tu. Wamama wenye tatizo hili husifiwa kwa kuwa na staha!!!!!!!!.
DOMOZEGE ni mkaka ambae anaweza kumuona mdada anaempenda lakini kila akikutana
nae mdomo unakuwa mzito kujieleza
ishu yake, kinyume cha jina lenyewe DOMOZEGE si kwamba hawawezi kuongea, aa
wapi wanawezakuwa waongeaji saaaana lakini ikifikia kueleza hisia zao kuhusu
mdada wanaempenda akili ina siz. Si mara moja domo zege hunyang’anywa tonge
mdomoni. Cha ajabu wakishanyang’anywa eti ndio wanaanza kufunguka,’Ohh unajua
anti mi nilikuwa na mipango mingi sana na wewe sasa naona bradha kaniwahi’, na
mara nyingi hujibiwa,’Jamani kwanini hukusema?” Kutokana na tatizo hili kuwa
kubwa, maana kipimo cha ukubwa kinakuja kutokana MADOMOZEGE siku hizi
wamechukua staili ambayo inaleta fujo kwenye fani, wameanza kumwaga zawadi za
bei mbaya. Utakuta DOMOZEGE anatoa iPhone5 mtaa huu, mtaa mwingine BB, kule
chini anamwaga minoti tu eti ndio iongee kwa niaba yake, au siku hizi kuna
staili ya kununulia watu Verosa, sasa huu ni ukorofi katika fani. Shule maalumu
kwa ajili ya MADOMOZEGE zinaanzishwa ili kuwa saidia wenzetu hawa, na kutokana
na maendeleo kutakuwa pia na masomo kwa ajili ya akina mama ambao wanaona nao
UDOMOZEGE unawakwaza. UMEONAEE
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE