Kutokana na maendeleo ya shughuli za mawasiliano ni vizuri
polisi nao wangekuwa na namba ya
customer care kama zile za ile kampuni ambayo ni bingwa ya kupoteza netwek na
zile nyingine unaonaee. Kwa mfano mtaani kwenu kuna kuwa na jambazi
unapiga 112 halafu mdada mwenye Kiswahili
cha wadada waliokulia Marekani anakujibu,
KARIBU POLISI KASTAMA SEVIS, KWA KIINGEREZA BONYEZA 1,KWA KISWAHILI
BONYEZA 2, KWA KINGONI BONYEZA 3, KWA KIKWERE BONYEZA 4. ukiminya 1, kale
kamdada kanakwambia KWA AJALI ZA GARI BONYEZA 1, KWA WIZI WA SILAHA BONYEZA 2,
KWA WIZI MDOGODOGO WA VIBAKA BONYEZA 3, KWA MATATIZO YA UGOMVI WA MAPENZI
BONYEZA 5, KWA UGOMVI MWINGINE BONYEZA 6, KWA MAMBO YA KISHIRIKINA BONYEZA 7,
unabonyeza 2, kamdada kanakujibu KWA KUPATA MSAADA WA HARAKA PIGA 999.
Unaonaeee
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE