Chama cha Maboifrend Tanzania (CHACHAMATA) katika mkutano
wake mkuu wa 2012 kimeamua kufanya mgomo utakaoanza kesho tarehe 1.12.2012 na
kuisha 16.2.2013. Nia na madhumuni ya mgomo huu ni kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia
wanavyofanyiwa wanachama wake kwa kulazimishwa mambo ambayo kimsingi hayana
uhusiano wowote na mapenzi.
Imekuwa ni kawaida mageloflend wengi kudai vitu kama kununuliwa simu za bei inayozidi
hata mshahara wa boifrend wao, kisha baada ya hapo kudai kununuliwa muda wa
maongezi kwa haohao maboifrend, jambo ambalo linawaweka maboifrend katika
wakati mgumu wa kuhangaikia kutafuta pesa za simu tu. Kuna wageloflend wengine
hudai kupewa magari, na baada ya hapo kutegemea fedha ya petroli na matengenezo kutoka kwa waliowanunulia,
hii inatatizo kwani fedha nyingi za maendeleo ya wananchi zinabadilishwa
matumizi na kuwa matumizi ya hawa wageloflend. Kuna maboifrend waliolalamika
kuwa wanadaiwa matumizi lakini hawaruhusiwi kwenda kazini sasa hii ni wazi ni
tatizo. Tuna lipoti ya maboyfrend ambao wakati huu wako lumande, wengine
wamefungwa na wengine wameishiwa hawana hata hela ya kula kutokana na
kulazimishwa kutoa chochote ili penzi liendelee. Na ukiangalia yote haya hayana uhusiano wowote na mapenzi. Katika
mkutano huu tunaiomba selikali wakati boiflend anakuwa kizimbani kwa kukwapua
hela na aliyefaidika na ukwapuzi huo nae awe mshtakiwa mwenza. Hivyo basi chama
kimewaagiza makatibu wa vyama kuanzia vitongojini kuelekeza wananchama wao
wasitoe zawadi yoyote kwa mageloflendi wao mpaka siku mbili baada ya ile
sikukuu ya KITAPELI ya Valentine. Tunategemea kupata feed back toka kwa
viongozi wa ngazi za chini kuhusu utekelezaji wa hili. ONYO KWA WALE
WATAKAOKIUKA, CHAMA KITAFANYA KILA MBINU MUWAOE HAO MLIOWAPA ZAWADI hii itahakikisha unapata kifungo
cha kuwa na huyohuyo mmoja maisha yote, au kumchonganisha na mkeo tuone moto
unapowaka.
PREZIDA
CHACHAMATA
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE