Nimewashtukia,
nawaambia nimewashtukia ohooooo, tutaonana wabaya hayaaa. Kila mtu anajua
waBongo huwaga hawana noma wala nini kuhusu ubora, wanachojali ni kuwa kitu
kimewezekana, sasa hizi ishu mnazotaka kuanzisha sasa mi nadhani ni njama zenu
za kawaida za ufisadi tu unaonaee, eti ohh kuanzia sasa mtu ukiwa na lain yako
unaweza ukahamia mtandao mwingine ukiona ule wa zamani unazingua, sasa hayo
ndio maneno gani, halafu kwanini mmeona nimejikwaa kidogo ndio eti siku
hiyohiyo ndo mnaanza kupigia debe hiyo ishu? Mi nawashauri wa Wabongo wenzangu
jamani tusikubali kuburuzwa, hawa mafisadi tukiwaachia kesho watatoa amri eti
kwenye daladala lazima kuwe na AC, na hakuna ruksa watu kusimama, yaani hii
itakuwa dizasta kwenye biznes si mnaonaee, wote sie ni wabongo tunajijua haya mambo madogo madogo huwa wala
hatumaind sasa jamaa wanaanza mbali eti ooh namba moja unaweza ukahama mtandao.
Kesho wenye daladala mbovu wote na mitandao mibovu, vyama vya siasa vibovu,
hoteli mbovu, gest mbovu, tukutane jangwani kudai haki ya kuwa na huduma feki,
mbona simu feki ruksa? Tena eti kusudi wananchi wasipate gharama si mnaonaee
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE