Kasheshe
ni pale unapompa binti mzuri mjamzito
lifti kwenye gari lako, halafu anazimia. Kasheshe zaidi ni pale baada ya
kumkimbiza hospitali, anapewa matibabu na kujifungua na kudai aliyemleta
hospital ndie mwenye mimba. Ubishi mkali unazuka, na binti anang’ang’ania wewe
ndie mzazi mwenzie. Unakuja juu na kuomba vipimo vifanywe ukweli ujulikane.,
kasheshe linaongezeka utamu pale inapogundulika kuwa, si tu kwamba wewe si baba
wa mtoto yule bali huna uwezo kabisa wa kuwa baba. Hapo ndipo kasheshe
linafikia upeo wa juu kwani unaanza kujiuliza wale watoto watatu ulionao
nyumbani ni wa nani?

No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE