Dah kumbe kujua kusoma sio lazima faida. Tena mara nyingine
ni hasara. We fikiria uko katikati ya mji, unataka kujisaidia, hakuna choo cha
umma, unaona kakichochoro fulani uawahi unataka kujisaidi unakuta maandishi
makubwa, USIKOJOE HAPA. Unakuwa mdogooo, ungekuwa huji kusoma wala
isingekusumbua,ungemaliza shughuli yako na kutoka mwepesiiii. Una shida na mtu,
unamfuata kazini kwake unakuta kibao kimeandikwa usiingie hapa, unabaki
umezubaa nje unasubiri namna ya kuomba ruksa uingie, ungekuwa hujui kusoma
ungeingia na kumaliza ishu zako na kusepa. Sababu tummejua kusoma, vibao hivi
vya usikae hapa, usipite hapo, hakuna kazi, mbwa mkali, nyumba hii inalindwa na
umeme, vinatufanya tuwe waoga hata kama hakuna kitu. Iko haja ya kuanzisha
shule ya kufuta kujua kusoma na kuandika. Hii mifesbuk wala isingekuwa ishu
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE