25 December 2012
MERRY NEW YEAR TO YOU TOO ALSO PIA NAWE
Kwa kusema kweli NIMEPATA
SHOCK.......sikutegemea kabisa na wala sikufikiria wala kuwaza wala
kuota unaonaee. Ila nashukuru Xmas hii imenifungua macho masikio na
mawazo. Kumbe asilimia kubwa ya rafiki zangu ambao kila siku tulikuwa
tukiwasiliana kupitia txt za simu na hapa FB kwa Kiswahili kumbe ni
mahiri wa Kiingereza umeonaee. Sijui kwanini walikuwa wananificha uwezo
wao huo. Asilimia 98.34 ya salamu za
Xmass nilizopata zimeandikwa Kiingereza, jambo ambalo limenifanya niweze
kutetea popote duniani kuwa nchi yangu Kiingereza ni lugha ya kawaida
kabisa mtaani si unaonaee. Japokuwa salamu nyingine zilikuwa
zinanishangaza kidogo maana mwisho unakuta zimemalizika kwa jina la mtu
mwingine siyo yule aliyenitumia , lakini hilo siyo ishu UNAONAEE.
Nangojea za I wish you merry new year, si ndio ee?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE