Si rahisi kujua siku yako ya kifo, lakini kuna watu hupata
bahati ya kujua muda umefika. Hapa ni baadhi ya mambo ambayo yatakusaidia kujua
kuwa saa yako ya kifo imewadia…..
UTAJUA KUWA MUDA UMEFIKA..pale ambapo majambazi wenye silaha wameteka gari lenu wote mkaambiwa mtoe simu zenu, wewe ukatoa NOKIA tochi na
kumuhakikishia jambazi kuwa ndio simu unayoitegemea, mara Blacberry Bold
uliyoificha kwenye chupi ikaanza kulia
UTAJUA KUWA
MUDA UMEFIKA pale ambapo unawasha kiberiti kucheki kama kuna mafuta kwenye
jenereta iliyozima ghafla
UTAJUA KUWA MUDA UMEFIKA pale mpenzi wako anapokwambia,
“Ingia uvunguni mwa kitanda mume/mke wangu kaja”. Wakati uko uvunguni simu yako
ya Mchina inaanza kuita
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE