Kwa bahati mbaya kuna Wabongo wana roho mbaya, na mbaya
zaidi wanaweza kukuendea kwa mganga hata kijijini kwao ili tu usifanikiwe.
Lakini pia kuna ndugu huko kijijini kwenu ukienda kuwatembelea linakuwa kosa, wanaamua
kukupiga kitu mambo yako hapa mjini yanakwama kishenzi. Nimekusanya hapa baadhi ya mambo
ambayo ukiona tu yameanza kukuandama ujue kijijini kwenu wamekuendea kwa
mganga;
i.
Ukiona kila unapodownload kitu ikifikia 99% hakiendelei ujue tayari
ii.
Ukiona umenunua Blackberry kwa shilingi laki 7,
kesho yake unakuta duka jingine wanauza ileile kwa shilingi laki 3 na nusu ujue
wameshakushughulikia
iii.
Ukiona hata ukitumia pafyumu gani, kikwapa kiko
palepale ujue tayari
iv.
Ukiona watu wote wanatanua, na wewe ukafuata
ukajikuta unakamatwa peke yako ujue wameshafanya mambo kijijini kwenu
v.
Unaingia chumba cha intaview unajikuta umesahau
hata jina lako, hapo ujue tayari
vi.
Ukikosea ukajikuta umetumia super glue badala ya
matone ya dawa ya macho, hapo wameshakutwanga
vii.
Unakuta mchwa wamekula jina lako tu kwenye vyeti
vyako vya shule we nione jamaa wameshakuchapa

ha ha nimeipenda hii hasa no. 2
ReplyDelete