BAUNSA KALETA BALAA
Baunsa wa night club alienda kutibiwa mgongo kwa doctor.
DOKTA: Ilikuwaje mpaka ukapata mshtuko wa uti wa mgongo?
BAUNSA: Nilipoingia home alfajiri nikitokea kazini,nilisikia makelele
chumbani kwangu nikajua mke wangu yupo na mwanaume
mwingine,nikazama chumbani kwa spidi lakini sikumkuta mtu,mara
nikasikia mlango wa sebuleni umefunguliwa kwa fujo,nilipochungulia
kupitia
dirishani nikamwona mtu anakimbia huku anavaa
shati,nikachukua fridge nikamrushia nikiwa ghorofa ya tatu,hapo ndipo
niliposhtua uti wangu wa mgongo.......Alipomaliza tu kauli yake,akaingia
mgonjwa mwingine kaharibika kama kagongwa na gari.
DOKTA: Na wewe nini kimekusibu?.
MGONJWA 1: Nilisahau kuweka alarm asubuhi nikachelewa kuamka kwenda
kazini,kazi yenyewe niliajiriwa jana tu baada ya kukaa jobless kwa muda
mrefu,nikatoka nje huku navaa nguo,mara nikapondwa na fridge
kichwani.......Mara akaingia mgonjwa wa tatu akiwa na hali mbaya kuliko
waliomtangulia.
DOKTA: Na wewe nini tena Yarabi?
MGONJWA 2: 'Doctor,mimi nilikuwa nilitaka kufumaniwa nikajibanza ndani
ya fridge,mara ghafla lile fridge likabebwa na kutupwa kutoka ghorofa ya
tatu
mpaka chini
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE