Naitwa John Kitime,
nilianza kufurahia vichekesho mara baada ya kuzaliwa na kukuta watu
wazima kila wakinichukua walijitahidi kunichekesha kwa kuanza kuonea
lugha ambayo sijaijua mpaka leo, maana mara alikuja mmoja na kuanza
‘bujibujibujibujibuji,jigijigjigjigjijij, grugrugrugru’ na maneno
mengine ya ajabu nilijitahidi kuwavumilia nisiwacheulie maziwa lakini
baadae nikagundua heri niwe nacheka wakianza vituko hivyo, maana baada
ya hapo walikuwa wanajiona wanajua kuchekesha watoto
wachanga. Niliendelea kukua nikaanza shule nakukuta vituko vingi sana vya
kuchekesha, kama vile watu kujikojolea darasani, hili bahati mbaya
nililikuta linajirudia pia kuwakuta wakubwa wakijikojolea kwenye baa, na
kilabuni, ene way, nilimaliza shule na kujiunga na vyuo mbalimbali
nchini na huko nilijifunza utalaamu wa kunywa pombe na huko nilikutana
na watu wengi wenye kujua kuchekesha, kucheka na hata wasiojua
kuchekesha wakijitahidi kuchekesha, cha kushangaza si nikakuta wengine
hawajui kucheka kabisa, au wanaweza kucheka mahala pasipo na kichekesho
cha kuchekesha wachekaji.
Katika kiota hiki cha www.chekanakitime.blogspot.com , ntaweeleza mengi yaliyonikuta katika maisha yangu haya yaliyojaa furaha sana NAMSHUKURU MUNGU.
Pia mimi ni
mwanamuziki napiga gitaa naimba kwenye bendi, lakini huwa sichezi, sijui
kucheza, hasa Chacha ndio kabisa halafu siku hizi kuna hii inaitwa
Kwaito, wakati najitahidi kujifunza imeanza Azonto, jamani si mngoje japo nijuwe staili moja ndio
mbadili? Halafu huwa inanishangaza, mtu analipa kuingia muziki halafu
anacheza kuliko sisi wanamuziki jamani, mnajua mngepewa majembe mlime
badala ya kucheza mngesha maliza tatizo la njaa hapa nchini?
nimekukumbuka ulikuwa darasa moja na henry mdimu na nilikuwa nimekupita madarasa 7 ila sikuwahi kufaulu mpaka mkaja mkanikuta darasa hilo hilo ndio tukamaliza wote.....nakumbuka sana ilikuwa ni darasa la 7 A.........!!!
ReplyDeleteWe si ndio ulikuwa mtoto wa yule mwalimu mnoko aliyekuwa bingwa wa kukagua kucha? Nadhani nakukumbuka, uliwahi kuanguka toka kwenye mti ukaanza kulilia maji ya kunywa
ReplyDelete