Binadamu wakiudhiana mara nyingine huamua kutwangana ngumi.
Unapojikuta umeingia katika mtiti wa kutwangana ngumi, akili zako lazima
zifanye kazi haraka sana na maamuzi magumu au mepesi lazima yatolewe tena mara
nyingine bila kutoa nafasi ya ubongo kufikiri. Lakini je, ungekuwa ubongo wako
unafanya kazi kiserikali serikali ingekuwaje?
Kwanza baada kujikuta umeingia katika mtiti wa ngumi
ingelazimu Katibu Mkuu husika aite maafisa wake kuona faida na athari za kutwangana ngumi, kisha baada
ya kupata jibu hili ungelazimika kufanya maamuzi kama je ujitetee au la, na kuna matatizo gani kisheria ukiamua kujiunga kwenye hizo ngumi.
Ungeamua kujitetea ingelazimu uite maafisa wengine kutafiti madhara ya kupigwa hadharani, au
je kuna matokeo gani ukimtandika mpinzani wako ngumi ya kushoto, na je ataangukia
wapi? Na kama angeakukia jiwe na kichwa kupasuka je matokeo yake yangekua nini?
Na umma ungelichukuliaje hili? Hapo ndipo ripoti nzima ingetolewa na kujadiliwa kuona kama kuna sababu ya
kuendelea na ugomvi huo. Shida tu ni kuwa mwenzio asie na urasimu angekuwa kesha
kupa mkong’oto wa nguvu
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE