Swaga
za jamaa yangu aliyekaa Dar kwa muda mfupi sana sasa karudi kijijini;
WAMJINI:
Unajua msikaji Ulaya na Tanzania tofauti ndogo sana. Kama sisi huku Tanzania
hata kule wana timu mbili tu kubwa, Manjesta na Asno. Hawa Manjesta wamejenga
ofisi sao na kiwanja nje kidogo tu ya
Landan, unapanda fidaladala fiwili tu umefika. Aliyeanzisa timu ni
kababu fulani kachawi hako, uchawi
wake kanatumia bablish, wakianza kuchesa tu kanaanza kutafuna bablish, kakimesa
tu, ujue hapo mmefungwa. Na hawa Asno nao
wako katikati ya jiji, unajua Landan kama vile Daslamu tu hakuna
tofauti, kuna Manzese, Magomeni, Yombo, sasa hawa Asno wako Yombo ya Landan,
kuna fi Hais unadandia unamwambia tu konda, ‘Msaada Asno’, basi wanakususa
kwenye kiwanja chao, na hawa nao timu yao alianzisa babu moja anaitwa Asno
Wenga, nako kachawi hako, mwiko wake hakaruhusiwi kucheka, kakicheka tu mjue Asno
itafungwa. Nasikia mwaka jusi kalikuja mbaka Samunge kwa Babu wa kikombe, timu
ilikuwa inafungwa sana, kalipokunywa tu kikombe wacha timu ije juu.
WAKIJIJINI:
Bwana we muongo bwana umejuaje hayo?
WAMJIJI:
Si nilikwenda kutembelea mjomba, nikakuta ana TV, ukiminya namba 5 kwenye
kidude fulani inatokea DSTV, hapo unapata siri sote za mpira wa Ulaya.
Unajua
sisi tungekuwa tunawafwata wale tungefika mbali sana, we ujue wanatumiaga mpaka
uchawi wa mvuto, unawasaidia kujaza watu kwenye viwanja vyao, we acha bwana
jinywee tu huo ulanzi wazungu we waache bwana
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE