28 February 2013
CHONDE CHONDE NAOMBA USHAURI
Mzee Kitime tafadhali naomba ushauri katika
hili tatizo langu. Mi nadhani mke wangu si muaminifu, anafanya kazi
katikati ya jiji, huwa anachelewa kurudi nyumbani na kila siku anarudi
na taxi wakati najua mshahara wake hautoshi kugharamia hilo, wiki
iliyopita nilijaribu kugusa simu yake alikuwa mkali kwelikweli kidogo
aniue. Ni kweli sijawahi kumuonyesha dalili zozote zaidi kuhusu wasiwasi
wangu, lakini jana nilamua kumfuatilia
wakati anatoka kazini, nikajificha mahala ambapo ntamuona anapotoka
kazini, kweli nikamuona anatoka na mwanaume mmoja simfahamu, nikaona
niangalie saa ili nijue ni saa ngapi walitoka, si ndio nikagundua saa
yangu imesimama, saa hii saa yangu ni Rolex na saa za aina hii ni
expensive sana, alinitumia rafiki yangu toka Uswisi na kunambia ina
gerentii haitasimama kamwe, sasa unanishauri vipi, niitengeze hapa
nchini, au nimrudishie itengenezwe Uswisi au ninunue nyingine?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE