Trafiki kakuta bonge ya ajali, dereva na pasenja
mwanamke wamefariki. Wakati akiangalia angalia kakajitokeza kanyani, toka
uvunguni mwa gari kakawa kana ruka ruka. Trafiki akasema, ‘Ungekuwa unajua
kuongea si ungetuhadithia ilikuwaje’ Nyani akatikisika kichwa kuonyesha
kaelewa. Trafiki akauliza, ‘Ilikuwaje?’. Nyani akaokota kopo la bia na kuonyesha ishara ya kunywa,
polisi akasema ‘ Walikuwa wanakunywa?’ Nyani katikisa kichwa kukubali. Halafu
nyani akaonyesha ishara ya kuvuta sigara, askari akauliza, ‘Walikuwa wanavuta
bangi?’ Nyani akatikisa kichwa
kukubali, Polisi akauliza ‘Na nini kingine?’ Nyani akaonyesha ishara kuwa
walikuwa wanabusiana, ‘ He walikuwa wanabusiana pia?’ Nyani kakubali.
Polisi akauliza, ‘Sasa wakati wanakunywa pombe, wanavuta bangi, na kubusiana we
ulikuwa wapi?’ Nyani akaonyesha ishara kuwa yeye ndiye alikuwa anaeendesha
gari.

No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE