TOFAUTI YA WADADA WENGINE
NA WAKAKA WENGINE.
MDADA 1: Hello
mpenzi mambo
MDADA 2: Niko poa sweety, dah umenikumbuka mamii
MDADA 1: Yaani nimekumiss, nikaona nikupigie nikwambie leo
naja kwako
MDADA 2: Dah nitafurahi kitu, jamaa shosti navunja safari
zote nakusubiri
MDADA 1: Baadae sweety. Akikata simu tu MDADA 2, anamwambia mdogo wake
MDADA 2: Yule Malaya kafosi kuja kunitembelea sijui ana
umbeya gani? Au kaishiwa anataka nijee nimnunulie bia za bure, ataula wa chuya
halooooo
MKAKA 1: We mwendawazimu uko wapi?
MKAKA 2: Hii kali masikini umepiga? Mkeo kakuruhusu leo ?
MKAKA 1: Hivi kwanini hujafa watu tule pilau?
MKAKA 2: Kufa sifi na leo nakuja kunywa bia bili yako, haya
nikukute wapi?
MKAKA 1: Pale kwenye baa anayonywea baba yako, usipokuja
ntashukuru maana hela yangu itanitosha vizuri sana. Akikata simu tu MKAKA 1
anamwambia mkewe, yaani huyu jamaa, ni rafiki yangu toka utoto, tukikutana huwa
raha sana
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE