Mke
alikuwa anajua kuwa mumewe yuko safari na hatarudi kwa wiki nzima, akamkaribisha mpenzi kwake,
kwenye saa 6 usiku siku hiyohiyo mumewe akapiga hodi, mdada akamwambia mpenzi wake simama
hapo pembeni jifanye sanamu mengine niachie. Jamaa akasimama kama sanamu
mke akamfungulia mumewe na kumpokea mizigo na kumkaribisha ndani. Mume
akamuangalia yule jamaa kisha akamuuliza mkewe,' Nini hiki?'. Mke
akajibu,' Wamachinga walipita na masanamu wanauza na mimi nikanunua
moja'. Mume akajibu ,'OK'. Akaenda zake na kulala hadi kwenye saa 9 usiku
akaamka, akaliendea lile sanamu akaliambia,'Pole kwa mbu ndugu yangu,
heri uondoke zako mie mwenzio ishu kama hii imenikuta Mbeya kwa mdada mmoja anaitwa Flora, nikapigwa
na baridi siku mbili ndio nikaweza kuondoka. Haya ondoka, usiku mwema'
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE