Jamaa kaingia chuo katikati ya simesta kaishiwa akamuandikia baba yake
barua. 'Chuoni mambo mazuri sana, kuna maajabu hapa maprofesa hapa
wamegundua njia ya kufundisha mbwa kuongea, mlete BINGO na shilingi laki
5, baada ya muda atakuwa anaweza kuongea. Mzee wa watu haraka akatuma
mkwanja na mbwa, haikuchukua muda mkwanja ukaisha. Denti akamtumia baba
yake barua nyingine kuwa wameboresha program sasa wanaweza kumfundisha BINGO kusoma, mzee aongeze kimilioni tu. Mzee wa watu aliyekuwa tayari
anajisifu kijiji kizima kuhusu mbwa wake anayeongea, akauza ng'ombe akatuma mkwanja. Likizo ikafika
Denti akabaki anawaza anaenda kumwambia nini baba yake kijijini. Alipofika tu kwao
baba yake akamuulizia BINGO. Denti akamuita baba yake pembeni,' Baba
hili nitakalokwambia sitaki mama asikie'. Baba akauliza,'Vipi tena?'.
Denti akaanza,' Ijumaa iliyopita tumeamka vizuri na BINGO, yeye kama
kawaida yake akaenda kuchukua gazeti la Ijumaa na kukaa kwenye kiti na
kuanza kusoma, ghafla wakati anasoma akaniita akanambia hivi, 'Baba yako
bado anaendelea na kale kachangudoa ka pale mtaa wa pili, naona hapa wameandika stori yake?', Baba kwa kweli nilishtuka'.
Baba akaingilia kati,'Ungemuua hapo hapo mbwa mshenzi huyu anataka
kuniharibia mambo yangu?', Denti akajibu,'Baba na mimi lilinijia wazo
hilohilo sikumchelewesha nikamtwanga nyundo ya kichwa'. Baba akamsifu
mwanae'Safi sana safi sana mwanangu, una akili sana
'
'

No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE