Tamko kutoka Chama cha Maboifrend Tanzania (CHAMATA)
Wapenzi wetu,
wake zetu, nyumba ndogo zetu, samsing zetu, dogodogo zetu, kutokana na sababu
zilizo nje ya uwezo wetu kama vile;
·
uchaguzi wa Madiwani katika kata 27
·
moto uliotokea mara kadhaa katika masoko ya
Mbeya
·
majukumu ya mambo ya shule mwezi January
·
vipigo visivyoisha vya Manchester United
·
ukijumlisha na kipigo kibaya cha Arsenal dhidi
ya Liverpool wiki iliyopita
·
kuhamishwa wa viongozi wa polisi karibuni
·
mtafaruku wa Zitto Kabwe na CHADEMA
·
vita vya Sudan Kusini
·
kuongezeka kwa rushwa
·
ujangili wa meno ya tembo
·
kukamatwa kwa shehena kubwa ya madawa ya kulevya
·
uteuzi wa Bunge la Katiba
·
kuongezeka kwa gharama za umeme
·
msongamano wa magari barabarani na mengine mengi sana
Tungependa kutoa taarifa mapema kwamba hatutashiriki wala
kuwepo katika sherehe za Valentine mwaka huu.
Nchi yetu inahitaji kufunga na maombi wakati huu, na sisi,
kama sehemu ya Taifa letu tumeamua kuwa katika mfungo wa kuombea nchi yetu
kuanzia tarehe 12 hadi 16 February mwaka huu. Tunashauri na nyinyi mchukue muda
huo mwafaka, kusherehekea Valentine na wazazi wenu kwani nao ni sehemu ya mapenzi ya
Valentine.
Tunategemea kukutana nanyi tena tarehe 17 na tunashukuru kwa
ushirikiano ambao tuna uhakika mtauonyesha katika kipindi hiki kigumu cha
kuliombea taifa letu Tanzania
MWENYEKITI TAIFA
CHAMATA
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE