ENYI BINADAMU NISIKILIZENI…. Siku
hiyo itakapofika.Siku ya kumi na nne ya mwezi ule wa pili wa mwaka, patatokea
miujiza mingi……..
Hakika nawambieni ghafla wale wanadamu wenye
simu za mkononi watawaambia maneno haya wenzi wao;
Nisamehe nisamehe kwani sikupatikana simu yangu ilionyesha Battery Low. Na wengine watasema, Nisamehe nisamehe sikupiga kwani
salio langu lilikwisha, na wengine watalia na kusaga meno wakiwambia wenzi wao,
Nisamehe nisamehe kwani bosi wangu alinituma safari ya Mkoa ya ghafla. Kutakuwa
na wengine wakisingizia magonjwa na ajali za ajabu na matatizo mengine hata
kufiwa. Wengi hawatonekana na wenzi wao siku hiyo. Lakini furahini nawambia kwani alama hizi zitapotea iingiapo siku ya
kumi na tano ya mwezi wa pili wa mwaka, Hakika hakika nawambia maneno yangu
yatatimia.Ole wao watakaongoja na kukesha na kutegemea kualikwa kwenye karamu
zenye vinubi na na mvinyo, wekeni
akiba pembeni ili muweze kujitegemea msije lia na kusaga meno........Joni Mblogaji 14:2
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE