Fisadi
kaiba mkwanja akaona itakuwa soo akiuweka benki maana siku hizi mtu
hata ukiweka hela zako Uswisi watu wananusa, akanunua sanduku akazisunda
zile pesa, akaenda msitu wa Mabwepande akatafuta mti mkubwa akachimba
shimo chini yake akafukia mkwanja. Ili awe na kumbukumbu akapiga picha
ule mti akaondoka zake kuwahi ndege maana alikuwa kwenye msafara wa bosi
mkuu. Akiwa hewani akaanza kuzicheki picha za ule mti aliofukia mkwanja
wa wizi, duh kucheki picha vizuri si akamuona mtu yuko juu ya ule mti amtoa bonge ya tabasamu,
mkojo ukamtoka palepale kwenye kiti cha ndege bila breki
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE