Luninga
aka TV aka Kibimbifukibambafu kidanganyawatu ni kitu moja hatari sana. Siku
hizi Kibimbifu ndio kimekuwa shule ya kila kitu. Kuvaa, kuongea, kuimba,
kucheza, na siku hizi mpaka kulea.
Watu
wanatengeneza video za singo zao kwa kukopi na kupest zile walizoona kwenye Kibimbifu,
hata muvi zinatengenezwa baada ya wajanja wetu kuangalia muvi kwenye Kibimbifu,
kasha kukopi na kupesti za kwao. Ila kali sasa ni wale jamaa zangu wanakopi na
kupesti namna ya kulea watoto wao kwa kujifunza kwenye Kibimbifu.
Juzijuzi
nilimtembelea rafiki yangu ambaye anajitahidi kuishi kama wale anaowaona kwenye
Kibimbifu, sasa yeye ana kavulana kake kako nasari, nako anakalea kama vile
vitoto vya kwenye Kibimbifu, na kwa vile kule nasari kamejifunza kutamka Dadi
and Mami badala ya baba na mama, jamaa yangu anajiona mjaaaanja, basi Kabwamdogo hako hakakaripiwi wala
kukatazwa chochote, nilipata taarifa kuna siku kalimvua baba yake taulo
alipokuwa katoka bafuni tena mbele za watu, jamaa akaishia kusema tu, ‘No Junia
no, is bad” Na kucheka cheka huku akisifu, ‘Tatizo la huyu mtoto ni ana akili
za kikubwa” Ene wei siku hiyo jamaa akanikaribisha kwake, basi kwa kweli
ilikuwa kero, mara Junia kaleta mpira anaupiga mbele yetu anaangusha vitu,
anatupiga usoni na mpira anaangaliwa tu, ‘Junia no’, anapanda meza mara kabati,
jamaa zangu utadhani wamelogwa, wanakenua tu meno, ‘No Junia no” Mara mbili
hivi kakaniparamia na kutaka kunivua miwani yangu, ‘Kwa ustaarabu wa nyumba ile
na mie nikatoa ya kinafiki, ‘No Junia no’. Bahati nzuri mama Junia akaingia jikoni, Baba Juni akaenda
chumbani kidogo, sebuleni tukabaki mimi na hiki kidude kisichokuwa na chembe ya
adabu. Si kikaanza vimaswali vya maudhi,’Leo umekuja kula kwetu?” ‘Kwenu mna TV? Babako anakuleteaga
chokoleti?” Kikawa mara kivunje kikombe mara glasi, mama yake anapiga kelele
toka jikoni, ‘Junia yu a veri bed’. Ila chenyewe kikakosea kikanipanda kichwani
na kuanza kunivuta nywele nikaona sasa hii zarau. Basi nilikishika mkono
nikakitolea macho na kukifinya vizuri mgogongoni. Kwanza kilitoa macho kama
kinataka kufa, kikaniangalia hakiamini akili yake kuwa kimefinywa na binadamu
aliye hai, na mie nikakiambia kwa sauti ya chinichini,’We Junya ukinisogelea
tena nakukata masikio’ E bwana we
kilitimka mle sebuleni mkojo unakitirirka kikaelekea jikoni. Kufika huko
nilitegemea kianze kulia kwa nguvu, kikawa kimya. Mama yake anakiuliza ’Junia
umefanya nini tena baba?’ kimya
“Junia what has happened?” kimya, mama yake akaja huku chenyewe kimejificha
nyuma ya gauni la mamake, ‘Huyu
kafanya nini?’ Nikajibu kwa sauti ya mtu asiye na dhambi kabisa, ‘Wala sijui
nimeona tu katimka hapa kaja huko’ Baada ya hapo kukawa na displin mle ndani
tukala na kuzungumza bila fujo. Baba Junia kila mara akimwangalia mwanae na
kumuuliza, ‘Junia a yu sik? Unaumwa?” Junia akinitupia jicho mwenyewe alikuwa
ananyamaza anajua kuna kukatwa masikio. Wengine hatuangaliagi Kibimbifu ohooo
Hahahah hii nimeipenda Uncle,
ReplyDeleteMe nge mtia makwenzi kabisa...