Juzi kwenye hivi vipindi
vya TV ambavyo wadada wameshika hatamu kutangaza, na huwa wanawauliza
watu mambo mengi tu nilisikia kali. Mdada alikuwa kamkaribisha daktari
wa hospitali wa wagonjwa wa akili, ambaye alielezea kuwa mtu anaweza
akaonekana mzima kabisa , lakini ukimuuliza maswali fulani rahisi
ukaweza kujua kuwa mtu huyo ana matatizo ya akili;
MDADA: Daktari unaweza kutufahamisha ni maswali aina gani?
DAKTARI: Kwa mfano naweza kumuuliza mgonjwa swali la kihistoria kwa mfano nikasema,'Dr Livingstone alifanya safari tatu kwenda Ujiji na ndipo kifo kikamkuta, sasa je ni katika safari ya ngapi alipofariki?'
MDADA: (kwanza alicheka kidogo) Watazamaji hayo ndio aina ya maswali ya dokta, mimi kwa kweli sikuwa mzuri sana kwa historia wakati niko shule, sina jibu ila nategemea watazamaji kuna wengi mmekwishapata jibu....sasa dokta huwa hamna maswali rahisi yanayohusu jamii tuliyonayo leo? (....nikahamisha chaneli)

No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE