WADADA STYLE
MDADA 1: Hello
mpenzi mambo
MDADA 2: Niko poa sweety, dah umenikumbuka mamii
MDADA 1: Yaani nimekumiss, nikaona nikupigie nikwambie leo
naja kwako
MDADA 2: Dah nitafurahi mno mpenzi, shosti navunja safari
zangu zote nakusubiri
MDADA 1: Basi baadae sweety tutaonana...........Akikata simu tu MDADA 2, anamwambia mdogo wake
MDADA 2: Yule Malaya kafosi kuja kunitembelea sijui ana
umbeya gani? Au kaishiwa anataka nijee nimnunulie bia za bure, ataula wa chuya
halooooo
WAKAKA STYLE
MKAKA 1: We mwendawazimu uko wapi?
MKAKA 2: Hii kali masikini bingwa wa kubip leo umepiga? Mkeo kakuruhusu leo ?
MKAKA 1: Hivi kwanini hujafa watu tule pilau?
MKAKA 2: Kufa sifi na leo nakuja kunywa bia bili yako, haya
nikukute wapi?
MKAKA 1: Pale kwenye baa anayonywea baba yako, usipokuja
ntashukuru maana hela yangu ina masharti, hakuna kulipia masikini. Alipokata simu tu MKAKA 1
akamwambia mkewe,
MKAKA 1: Yaani huyu jamaa, ni rafiki yangu toka utoto, tukikutana huwa
raha sana, ngoja nikamtukane hukohuko bar.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE