Baada ya tetesi kufikia blog hii kuwa wadada wasanii
wamekuwa na tabu kweli kuwataja
wapenzi wao kwa kuogopa kuibiwa , blog hii ilimtuma mwandishi wake
mahiri akajaribu kupata ukweli kuhusu hili.
MWANDISHI: mambo sister
MDADA: Poa tu jamani nani mwenzangu?
MWANDISHI: (Akitoa kitambulisho chake ambacho sijui kapata
wapi) Dada mimi ni muandishi wa lile gazeti mashuhuri la mtandaoni ambalo
limeapa kusema ukweli daima kama inalipa. Niliomba nikuhoji, kwa kuwa gazeti
letu linasomwa mpaka Ulaya , hii itakuwa promo sana kwako
MDADA: Ai weweeeee, ehe unataka kujua nini? Maana mie
sijatoa muvi wala singo muda sasa
MWANDISHI: Kiukweli mimi nilikuja kujua kuhusu maisha yako,
unajua nyie masupastaa, watu hutaka kujua maisha yenu, sasa tumeambiwa una
jumba la kifahari kama la Rihanna tulipenda wafuasi wako wajue
MDADA: Is true. Nina nyumba ya kifahari hapo Tandale kwa
Mtogole, ina choo cha kifahari, bafu la kifahari, sebule na korido ya kifahari na jiko la
kifahari. Kila chumba kina TV mbili na redio moja
MWANDISHI: Safi sana, sasa hii nyumba umepanga shilingi
ngapi?
MDADA: Nyoooooooooo unaona shepu ya kupanga hii?
Nimenunuliwa na bwanangu mpya. Tunaoana karibuni, harusi yetu itakuwa
Palestina, tutasindikizwa na Mashauzi Classic Taarab
MWANDISHI: Ohh hongera sana. Umempa nini mpaka akakununulia
nyumba hii?
MDADA: Unauliza makofi polisi hahahahaha
MWANDISHI: Okay. Nadhani wafuasi wako wangefurahi kumjua
huyo anayemtunza supasta wao , unaweza kunambia jina lake?
MDADA: Hilo hapana haliwezekani
MWANDISHI: Kwanini? Mganga kakukataza?
MDADA: Oh no, mambo ya waganga baadae kidogo, ila bwana huyu nikimtaja tu wenzangu wataniibia
MWANDISHI: Hayo matusi sasa, ina maana kuwa wadada wa hapa
mjini wezi namna hiyo?
MDADA: Habari ndio hiyo
MWANDISHI: Labda niulize kitu dada, huyo bwana wako zuzu
kiasi gani hata akununulie nyumba halafu kesho aibiwe kama mzigo wa kuni?
MDADA: Wanawake hasa wasanii wabaya watamshawishi tu.
MWANDISHI: Kwa hiyo, usiri huu utaisha lini, maana
akijulikana tu watu watachukua mzigo, hata kama mmeshaoana
MDADA: Bwana ee ngoja nikwambie ukweli, hii nyumba wanachangia
pango wanaume wengi, sasa nikimtaja mmoja hao wengine itakuwaje si watakimbia?
Kwa hiyo sisemi kitu ili kila mmoja kwa kuwa hawajijui anaona ye ndio mjanja
MWANDISHI: Okay sasa ninaanza kuelewa, Kumbe ndio staili
yenyewe?
MDADA: Mjini hapa kaka ukiwa na bwana mmoja si atachoka
kulipa bili
MWANDISHI: Okay mdada siri yenu simwambii mtu bye
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE