Kutumia
dawa za kulevya sio ujanja kabisaaa. Ni mtego ambao ukiingia kutoka sio rahisi.
Dawa za kulevya zina haribu kabisa taratibu za maisha, vijana wengi hawataweza
tena kufikia kiwango chao cha mafanikio katika maisha kutokana na kuingia
katika janga hili, kwani malengo ya maisha hubadilika kukawa na lengo moja tu,
nalo ni kupata pesa tu ya kununua dawa nyingine ili kulewa tena na tena.
Usikubali kuingia katika mtego wa dawa za kulevya.
Ila
vituko vya watumiaji wa dawa za kulevya ni vingi mno. Wakati niko sekondari
kuna mwenzetu mmoja alifanya maajabu makubwa. Ilikuwa ni wakati wa mapumziko ya
saa nne asubuhi, akawakuta rafiki zake wako chooni wanavuta bangi nae siku hiyo
akaona aonje huo moshi. Mwanzo hakuona tofauti yoyote mpaka pale alipoingia
darasani. Akiwa kimya anafuatilia masomo mara akahisi kuwa kuna siafu wameingia
ndani ya shati lake, akapiga ukelele na kuanza kuvua shati huku akilalamika ‘Siafu
siafu’. Darasa zima tukashtuka na kuanza kumuangalia, alipomaliza kuvua shati
akilalamika kuhusu siafu ambao sie wengine tulikuwa hatuwaoni ghafla akadai
wamehamia kwenye suruali na kuivua suruali, ilichukua muda mfupi wenzie
aliovuta nao bangi wakatambua kuwa kuwa ni matokeo ya bangi, si ndipo minong’ono
ya bangi ikaanza kuzunguka darasani watu wakaanza kucheka badala ya kumhurumia.
Ndugu yetu akatimka nje ya darasa kukimbia siafu aliokuwa akiwaona yeye peke
yake. Suruali na shati akiwa kaviacha darasani. Wanafunzi waliokuweko nje
wakaanza kumfukuza na hatimae kumkamata, wakati huo akawa kabadili maneno,
akawa analalamika kuwa mawingu yanashuka. Akawa na anaangalia juu na kulalamika
kuwa mawingu yanashuka yatamgandamiza. Shule nzima ilikuwa imepata habari kuwa
mwenzetu kavuta bangi sasa inamletea aluweluwe. Akapelekwa kwa mwalimu mkuu
huko akabadilika, akaanza kumkumbatia mwalimu mkuu aliyekuwa mama mtu mzima na
kudai ni valentine wake wa siku nyingi. Ilikuwa kazi mwalimu kujaribu kujinasua
kwa kijana ambaye alikuwa kavaa bukta tu
aking’ang’ania kuwa anamkumbatia valentie wake. Hatimae akafungwa kamba
mikono nyuma japo aliendelea kucheka na kudai mambo mbalimbali mara akijitetea
kuwa yeye ni Rambo na ataweza kujifungua mara alalamike kuwa yeye mfungwa wa
kisiasa. Ila jambo moja ni kuwa kuanzia siku ile aliapa hataonja tena dawa za
kulevya za aina yoyote maishani mwake.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE