Ndugu
zangu nawaombeni msaada maana kuna rafiki yangu anakesi kali sana kwa mkewe na
anaomba eti niwe shahidi yake. Ila nina wasiwasi yaliyomkuta nikiyatetea yatavunja ndoa yangu ambayo
ni miaka mingi. Ukija mtaani kwangu uliza mtu yoyote atakuambia kuwa mimi ni
mtu mtaratibu, nampenda mke wangu na haya mambo sijui ya kuchepuka, mimi sina
kabisaaaa. Kifupi mimi ni mfano mzuri kwa ndoa za siku hizi. Sasa kilichomtokea
rafiki yangu nikikikubali kitatishia kuvunja misingi imara ya ndoa yangu niliyojenga
siku nyingi.
Hii
mvua inayoishia ndio chanzo cha tatizo. Yaani nimechanginyikiwa kwa kweli. Kwa
kadri ya maelezo ya rafiki yangu, eti siku nne zilizopita alitoka kwake na
kuelekea dukani maana alikuwa amejifungia ndani muda mrefu na mkewe sababu ya
mvua, hivyo ikawa lazima atoke aende
kununua majani ya chai na sukari. Wote mnajua mvua zilivyochachama siku mbili
tatu hivi, kabla ya kufika dukani kulikuwa na mtaro mrefu, anasema alivyoruka
kumbe hakupiga mahesabu vizuri nikajikuta ametumbukia kwenye maji yaliyokuwa
yanaenda kasi, akasombwa na maji. Baada ya hapo anasema hajui kilichotokea ila
tu akajikuta yuko kwenye kitanda kwenye chumba hakifahamu. Mwenye chumba kuja
alikuwa binti mmoja mrembo aliyemwambia kuwa alizolewa na maji na kuokotwa na
wasamalia wema na binti huyo alijitolea kumpa pa kulala mpaka atakapopata nafuu.
Na akadai ilikuwa siku ya nne ndipo alipopata fahamu Tatizo na kuwa wambeya
walienda kumwambia mkewe kuwa wamemuona jamaa kwa mwanamke mmoja na mkewe akaja
kumkuta huko na kudai kamfumania. Yaani kila nikifikiria kumtetea hadithi hii napata
tabu kwani najua mke wangu atadhani tunashirikiana kutetea safari zetu. Naomba
msaada wenu nifanyeje ili stori hii ikubalike kuwa rafiki yangu kweli alizolewa
na mafuriko yakamtupa kwenye chumba cha mrembo. Nahitaji jibu mapema
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE