Mheshimiwa
mmoja baada ya kupata cheo si akapewa nyumba mitaa ya watu wenye pesa, akahamia
huko akiwa na mke na mwanae. Siku moja mwanae aliyekuwa kazoea maisha ya Uswazi
akawa anawinda ndege na manati kwenye uwanja wa jumba lao, bahati mbaya jiwe
likapitiliza na kwenda kuvunja kioo cha nyumba ya jirani. Mheshimiwa na mkewe
wakaamua kumfuata mwenye nyumba wakamuombe msamaha. Walipogonga mlango akafukua
mbaba mmoja akawakaribisha kwa heshima, wakaingia na kuanza kujieleza.
‘Samahani sie tumehamia karibuni hapo nyumba ya pili, mwanetu kavunja kioo
chako kwa bahati mbaya, tumekuja kuomba msamaha na kuona kama tunaweza
kutengeneza’. Mwenyeji wao akawaomba wakae kisha akawaambia, ‘Naomba
niwahadithie kitu. Kwanza mimi nawashukuru nyinyi na mtoto wenu. Mwenye nyumba
hii ni mchawi mkubwa sana, mimi ni ZIMWI alikuwa amenifungiwa kwa zaidi ya
miaka 200 kwenye kichupa ambacho kilikuwa kwenye dirisha lililovunjwa na chupa
nayo ikavunjika nami nimekuwa huru, kwa hiyo kwa shukurani ombeni chochote
mtakacho nitawapa, nina uwezo huo’ Hapo hapo muheshimiwa akauliza tena,’Yaani
kitu chochote?’ Akajibiwa ‘Ndio’. Basi pale pale akasema, ’ Mimi naomba niwe
bilionea mpaka nife’ Akajibiwa ,’ Hilo jambo dogo sana kwangu, umepata na kesho
utaamka tajiri’ Mama nae akaomba vyake, ‘Mi nataka niwe na nyumba kila nchi
duniani na niwe na biashara Dubai na China na HongKong’ Akajibiwa, ‘Umepata
mama, kuanzia kesho hayo ni yako. Mimi nawashukuru kwa uhuru wangu lakini nina
kaombi kadogo’. Mheshimiwa haraka akajibu, ’Sema tu wewe ni kama ndugu yetu
sasa’ Basi ZIMWI likasema, ‘Naomba mkeo abaki hapa kama masaa mawili tu, unajua
kifungo nilichofungwa kilinizuia kila kitu, hata mke sijapata kipindi chote
hicho. Nikimaliza tu hilo ntaondoka kurudi kwetu Uzimwini hamtaniona tena,
itakuwa siri yetu’. Mme na mke wakajadiliana wakaona utajiri waliopata ni
mkubwa sana, na hilo jambo ni dogo sana la mara moja tu tena kwa siri,
wakakubali sharti. Mke akabaki pale kwa masaa kadhaa. Shughuli ilipokwisha,
mama wa watu akiwa anajitayarisha kurudi kwa mumewe kichwani akiwaza utajiri,
ZIMWI likakohoa kidogo na kumuuliza yule mama, ‘Samahani una miaka mingapi na
mumeo ana miaka mingapi?” Mama wa watu akajibu, ‘Mie nina miaka 40 mume wangu
ana miaka 46’ Yule Mbaba akacheka sanaa, ‘Sasa nyinyi wakubwa wazima mpaka leo
mnaamini stori za MAZIMWI?
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE