Unajua
Mbongo wa kawaida akipata kesi anapaniki, Atajaribu kila njia kumaliza kesi nje
ya mahakama, ikishindikana huanza kutafuta ndugu na marafiki wampe ushauri
afanye nini? Amuone nani? Hapo ndipo ataliwa pesa na ndugu na rafiki zake na
kusitokee msaada wowote. Akistuka basi ataanza kumtafuta polisi aliyeshika
kesi, na akiona huku kumeshindikana basi utasikia kagonga hodi kwa mganga na
kuomba dawa ya kufuta kesi, eti kesi
yake ifutike kimiujiza, hapo ataliwa tena mkwanja wa nguvu, kuku kadhaa
watapoteza maisha na kesi huwa inaendelea, na inaweza ikaishia jamaa akafungwa
kirahisi tu. Sasa mimi nina kesi mbili nimeshtakiwa , lakini nasubiri kwa hamu
kwenda mahakamani tena nitawahi mimi kabla ya walalamikaji. Kesi zote zinahusu
kuharibu mali za watu. Hii ya kwanza ilinikuta pale Mwenge, nilikuwa nimeazima
gari la baba mdogo napiga misele si nikajikuta kwenye barabara inayopita
katikati ya ilipokuwa stendi ya Mwenge. Kuna jamaa wenye akili za kiajabu ajabu
wanabiashara ya kuuza viatu vya mchuchumio, hao wamepanga viatu vyao mpaka
barabarani, na wanategemea gari zikwepe viatu vyao. Sasa nilipofika hapo ikawa
tupishane na daladala, barabara imekuwa nyembamba, ningekwepa viatu ningepigwa
pasi na daladala, nikaona sipendi ujingaujinga, nikavikanyagilia mbali viatu
vya mchuchumio vilivyokuwa barabarani. Jamaa wakaanza kelele na vurugu na ndio
wamenishtaki kwa kuharibu mali yao,
nimesema nawahi mahakamani kabla yao. Kesi nyingine imenikuta eneo la
Shekilango, serikali imetengeneza barabara ya kisasa, ina njia ya watembea kwa
miguu na njia ya kwa ajili ya bodaboda na baiskeli. Jamaa wanaojifanya akili
zao hazina akili wamepanga bidhaa zao na kuziba njia ya bodaboda na baiskeli,
watembea kwa miguu na bodaboda wanalazimika kututumia njia moja. Mi nimepitisha
bodaboda yangu katikati ya mali zao walizopanga kwenye njia ya bodaboda,
sikuona sababu ya kuwasumbua waenda kwa miguu kwenye njia yao sababu ya
wakorofi wachache. Jamaa wamenishtaki nimetangulia mahakamani nawasubiri
sipendi ujinga mimi.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE