Msomi mmoja alikuwa anafanya utafiti, akamchukua chura akamwambia 'Ruka',
chura akaruka mita 4, msomi akaandika katika kitabu chake kuwa chura
mwenye miguu minne huruka mita 4. Kisha akamkata mguu mmoja na kumwambia 'Ruka'
chura akaruka mita 3, msomi akaandika kuwa chura mwenye miguu mitatu huruka
mita 3. Akamkata mguu mwingine na kumwambia aruke , chura akaruka mita 2,
akaandika kuwa chura mwenye miguu miwili huruka mita 2, kisha akamakata mguu
mmoja, na chura akaruka mita moja, msomi akaandika chura mwenye mguu mmoja
huruka mita moja. Hatimae akamkata mguu wa mwisho, na kila alipomwambia 'Ruka'
chura hakuruka, msomi akaandika kuwa katika utafiti wake amegundua chura
akikatwa miguu yote huwa anakuwa kiziwi.

No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE