DOGO: mama naomba nikalale kwa akina Helena, mama yake
amesema ataturuhusu tulale chumba kimoja mmoja juu mwingine chini
MAZA: Kasema nini? Mshenzi mkubwa huyo, hebu twende…. Maza
akafunga kibwebwe tayari kwa valangati
MAZA: We mama Helena mbona huna akili kwanini unataka
kuniharibia mtoto wangu mshenzi mkubwa wewe?
MAMA HELENA: Jamani kwani nini?
MAZA: We umesema watoto waje kwako wakalaliane ndio nini?
Mwanamke huna haya weweeeeeeee
MAMA HELENA: Jamani
we mtoto mi nimekwambiaje
DOGO: Umesema nije nilale kwenu na Helena, moja juu mwingine
chini.
MAMA HELENA: Jamani Mama Dogo, kuna kitanda cha ghorofa
mtoto moja analala juu mwingine chini haaa mwanamke weweee.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE