29 June 2012

Toka Magazetini ndani ndani kabisa


Kizimbani kwa wizi….Nipashe

Na Mwandishi wetu

28th June 2012



Mfanyabiashara, Ajastina Kabume (23), amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa kosa la wizi.

Mwendesha mashitaka mratibu wa Polisi, Denis Mujumba, alieleza mbele ya Hakimu, Karimu Mushi kuwa majira ya saa 12 maeneo ya Tabata Liwiti manispaa ya Ilala, mshitakiwa aliiba vitu vyenye thamani ya Sh. milioni 1,399400 mali ya Priscus Venanc.

Mshitakiwa amekana shtaka hilo na yuko nje kwa dhamana na kesi yake imeahilishwa hadi Julai 11, mwaka huu itakapotajwa tena……….Hapa wahusika walikuwa wamechoka maana kuna makosa kibao humu, kubwa ni  hii mali walioyoiba walibebaje? Labda na meli kadhaa………milioni 1,399400 duh mwanawane



Toka Mtanzania
SUALA la uadilifu kwa watumishi wa umma, limendelea kushuka baada ya watumishi wa Serikali katika Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma kujiuzia magari ya Serikali aina ya Land Rover 110 kwa Sh milioni 2, huku thamani ya gari hilo ikiwa ni zaidi ya Sh milioni 120.
Mbali na gari hilo ambalo linadaiwa kununuliwa na mmoja wa watumishi katika Wilaya ya Kibondo, gari jingine limenunuliwa na Mwanasheria wa Wilaya, D. Ruhamvya, aina ya Nissan Patrol lenye namba za usajili SM 2976 kwa Sh milioni 3…….Sisemi kitu mamana sijui hali ya gari ilikuwaje. Pengine wamenunua scrapper?



Toka Tanzania Daima
MBUNGE wa Micheweni, Haji Khatib Kai (CUF), amesema kuwa mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa zikilalamikiwa kwamba zinachochea vitendo vya zinaa kwenye vituo unavyopiga kambi…………Mhhhhhh haya tena, itakuwa lile joto la Mwenge

Toka Tanzania Daima
HOSPITALI ya Regency ya Dar es Salam imeanzisha programu kabambe ya upasuaji wa maradhi mbalimbali ya tumbo kwa njia ya teknolojia ya kisasa ya kutumia kamera……….Dah nawaza tu picha za utumbo wangu ziki 'wikiliki' kwenye magazeti ya makorokocho

No comments:

Post a Comment

SEMA USIKIKE