Ufisadi unatajwa sana
katika mali kama ardhi, na pesa. Utasikia watu wanalalamika ohh Mwenyekiti
anahodhi eneo kubwa sana la ardhi peke yake wakati wengine hawana eneo, au ohh
jamaa anahodhi akaunti kubwa ya vijisenti wakati wananchi wengine wakiwa hawana
hata hela ya kula. Kuna ufisadi ambao uko wazi ila watu wanaukwepa kuupiga
vita.
Sensa ya mara ya mwisho
hapa nchini, ilionyesha wazi kuna
uhaba mkubwa wa wanaume hapa nchini, sasa unakuta wamama wanahodhi mwanaume na
kukataa katakata kushirikiana katika matumizi kwa ushirikiano na wamama wenzie, huu ni ufisadi wa hali ya
juu. Acheni uchoyo, tumieni bidhaa hii adimu kwa ushirikiano, amani na upendo. Nawasilisha hoja
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE