Jumuiya ya Madikteta
tumeamua kutoka hadharani kuwatetea wanyonge. Nyie wanyonge mnapata tabu sana
kwa hiyo sisi tumeamua kuwatetea. Tuna mikakati kabambe ya kuhakikisha
mnakombolewa kutoka hili dimbwi la njaa kali, uonevu, dhuluma, na kunyimwa haki
zenu za kimsingi kwa ujumla. Ili kuweza kuwaletea raha ya milele tutafanya
yafuatayo;
1. Tutazuia chakula
kisipikwe popote (mnajua hili ni kiboko maana wanaowanyanyasa wakiona mna kufa
kwa njaa watapanik, hivyo watapanga mikakati ili chakula kipikwe)
2. Tukiona kuna dalili
za chakula kupikwa mahala fulani tutafanya chini juu mpango huo usifanikiwe ili
muendelee kufa kwa njaa, msingi hapa ni ‘objective’ kufa mtu mmoja hapa na pale
siyo main issue. Tunajua mtatuelewa na mtakuwa na sisi katika kipindi hiki
kigumu cha kutafuta njia ya kuwapa raha ya milele, mpaka tone lenu la mwisho la
damu.(hapa tuwapongeze wapishi wote waliogoma kupika, maana wakifa watu wengi ndo ushindi wetu utakaribia)
3.Jumuiya ya Madikteta
tungependa kuwataarifu kuwa ‘off course’ na sisi tuna kitu tutapata katika
kuwakomboa, maana hatimae tutakuwa na magari, mishahara mikubwa, nyumba za
kisasa, likizo Ulaya, lakini hivi ni vitu vidogo sana kulinganisha na ambacho
hatimae mtapata maana itakuwa raha ya milele, hakuna kufa wala nini mtaishi
mpaka mchoke
4.Tuungeni mkono kwa
kuonyesha kuwa mnateseka na kufa wengi kwa njaa kwenye vyombo vya habari, hii
itasaidia sana watu kushika adabu na kutuachia tupate tunachotaka, yaani
furaha na raha yenu ya milele bila kufa
IMETOLEWA NA MPASHA HABARI WA
JUMUIYA YA MADIKTETA
DUNIANI KWETU
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE