5 July 2012

Je 2+2 ni ngapi?

Kulikuwa na tangazo la kazi, watu watatu, mwanafuzi, mhasibu, mwanasiasa wakapeleka maombi, siku ya usaili wakafika tayari kwa usaili;
MSAILI: Je 2+2 ni ngapi?
MWANAFUNZI: 4
MSAILI: Haya nenda niitie mwenzio
MSAILI: Je, 2+2 ni ngapi?
MHASIBU: Kwa ujumla ni 4, inaweza ikazidi kidogo au kupungua kidogo kwa asilimia kama 10 hivi lakini ni 4
MSAILI: Du haya nenda niitie mwenzio
MSAILI: Je 2+2 ni ngapi?
MWANASIASA: (Kwa sauti ya chini) We unataka iwe ngapi bosi?

No comments:

Post a Comment

SEMA USIKIKE