Ndugu Mhariri,
Nimeona niandike kwenye gazeti lako ili unisaidie katika
tatizo langu, maana kwa kweli nimeona umesaidia wengi wenye matatizo kama
yangu. Juzi nilikuwa naenda kazini nikamuacha mume wangu nyumbani anaangalia
TV, gari langu likazima kama kiasi cha kiliomita moja toka nyumbani. Nikaona
nitembee mpaka nyumbani kumwomba mume wangu aje anisaidie kutengeza gari. Kwa
msahangao wangu nilipofika nyumbani nikamkuta mume wangu yuko na chumbani na msichana
wa kazi wa nyumba ya jirani. Mume wangu ana miaka 43, mimi nina miaka 39 na
msichana huyo ana miaka 19 hivi.Tumekuwa katika ndoa kwa miaka 10.
Nilipomuuliza mume wangu alikubali kuwa uhusiano wao umekuwa ukiendelea kwa
miezi sita sasa, nifanye nini mimi?.
Wema
Jibu
Dear Wema,
Nimesoma vizuri barua yako na naweza kukushauri ifuatavyo, kwa
kusema ukweli gari kuzima ghafla linaweza likawa limesababishwa na mambo kadhaa,
aidha betri haichaji, au petroli imekwisha au fyuzi imekatika Ni vizuri
ukaanaza kuangalia kama filta ya petroli ni safi na jaribu pia kucheki plagi.
Nategemea jibu hili litakusaidia
Mhariri
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE