4 July 2012

Mume wangu nikifa utaoa tena?

MKE: Nikifa utaoa tena
MUME: Hapana
MKE:Kwanini hupendi kuwa ndani ya ndoa?
MUME:Hapana siyo hivyo
MKE: Sasa?
MUME: Haya nitaoa
MKE: Mtakuwa mnakaa kwenye nyumba yangu hii hii?
MUME:Ndio
MKE: Mtakuwa mnatumia gari langu hilihili?
MUME: jamani gari bado zima nategemea tutalitumia hilihili
MKE: Na picha zangu ukutani mtazitoa?
MUME: Ndiyo
MKE: Mtalala chumbani kwangu humuhumu?
MUME: Ndio, jamani maswali gani haya?
MKE: Na madira yangu atakuwa anavaa?
MUME: Hapana ye anapenda kuvaa suruali........JAMAA YETU YUKO HOSPITALI ANAUGUZA VIDONDA VYA KUMWAGIWA MAJI YA MOTO

No comments:

Post a Comment

SEMA USIKIKE