2 July 2012

Toka magazetini leooo


Hadija Jumanne…Mwananchi
WAFANYABIASHARA wawili wa jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Ilala mwishoni mwa wiki kujibu mashtaka saba yakiwemo ya kughushi  na kujipatia Sh30.7 milioni kwa njia ya udanganyifu.
Pia washtakiwa hao wanadaiwa kughushi hati ya kiwanja namba 236 kilichopo eneo la Gezaulole Wilaya ya Temeke huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Washtakiwa hao ni Denis Ally (27) na Denis William (28) na walisomewa mashtaka yao yakiwemo ya kughushi kiwanja, kufanya utapeli na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu…………Nyie akina Denis nangojea hukumu yenu ya  kwa kosa la kugushi kiwanja  maan nyinyi mtakuwa watu wa kwanza kugushi kiwanja, how did you guys manage to forge a piece of land? Wabongo kiboko, hata mzungu hana jeuri ya kugushi kiwanja ujanja wake wote.
 *******************************************

Mwandishi Wetu, Dodoma-Mwananchi
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limefilisika, halikopesheki na linahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa……Duh kumbe mi nina thamani kuliko TANESCO? Mi nakopesheka, sasa Tanesco njoni tufanye dili, mi nikakope halafu niwakopeshe, ilamtanilipa kwa  riba, kama mko poa tuongee, njoni na kadi za gari kama mnazo tufanye mambo au vipi?

***********************************
        
Walimu walala madarasani Katavi
na Walter Mguluchuma, Mpanda (Tanzania Daima)
……haina noma mbona Wabunge wanalala Bungeni?
******************************************
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, amesikitishwa Tanzania kupoteza umaarufu wa soka ikilinganishwa na miaka ya 1970.
Sumaye alisema hayo juzi katika Hoteli ya Double Tree By Hilton ya jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuwatunuku washindi mbalimbali waliofanya vizuri kwenye Ligi Kuu ya msimu uliopita.
Alisema hiyo inatokana na klabu za Simba na Yanga kuridhika na moja kuifunga nyingine kama vile ndio mwisho wa mafanikio………bisheni tu kwa kuwa mmezoea kubisha Katavi Rangers wangepata dili hili leo tungekuwa tunashindana na Barcelona, maana wangekuwa wanawaza mbele zaidi
*************************************

No comments:

Post a Comment

SEMA USIKIKE